

Lugha Nyingine
![]() |
Watu wakizungumza kwenye hafla ya kitamaduni katika Kituo cha Utamaduni cha China mjini Cotonou, mji mkuu wa kiuchumi wa Benin, Julai 29, 2025. (Picha na Seraphin Zounyekpe/Xinhua) |
COTONOU – Shughuli ya kitamaduni imefanyika Jumanne usiku wiki hii katika Kituo cha Utamaduni cha China mjini Cotonou, mji mkuu wa kiuchumi wa Benin, ikiwapatia watu wa Benin ufahamu wa kina kuhusu urithi wa Xi'an, mji mkuu wa Mkoa wa Shaanxi na moja ya miji ya kihistoria zaidi ya China.
Ikiwa imeandaliwa kwa pamoja na Kituo cha Utamaduni cha China nchini Benin na Ofisi ya Utamaduni na Utalii ya Mji wa Xi'an, shughuli hiyo yenye kaulimbiu ya "Chang'an katika Mjongeo: Kunufaisha Urithi wa Utamaduni Usioshikika," ilikusanya pamoja washiriki karibu 200, wakiwemo wapenda utamaduni wa China, wanadiplomasia wa kigeni, na wanafunzi kutoka Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Abomey-Calavi.
Shughuli hiyo ililenga kuhimiza maelewano kati ya watu wa nchi hizo mbili kupitia ufahamu wa urithi wa utamaduni usioshikika wa China ambapo jambo muhimu la shughuli hiyo ilikuwa safari ya hisia nyingi kupitia Xi'an, moja ya miji mikuu ya kale ya China, iliyowezeshwa na vifaa vya kuvaa machoni kuonesha uhalisia pepe ambavyo viliwezesha watembeleaji kujionea maajabu ya kihistoria kama vile Mashujaa wa Terracotta wa Mfalme Qinshihuang.
Wanafunzi kutoka Taasisi ya Confucius walipanda jukwaani wakiwa wamevalia mavazi ya kijadi ya Hanfu, wakivutia ushangiliaji na shangwe kutoka kwa watazamaji. Wahudhuriaji pia walipata fursa ya kujaribu ufundi wa kijadi kama vile upakaji rangi za vinyago vya uso vya opera ya Qinqiang na utengenezaji feni za rangi nzito.
Wakati huohuo, kona ya chakula ilitoa ladha ya vyakula maarufu vya Xi'an, vikiwemo roujiamo (mkate bapa uliojazwa nyama) na liangpi (tambi baridi).
Kwa mujibu wa Videkon Dudedji Gwladys Gandaho, naibu mkuu wa wafanyakazi katika Wizara ya Utalii, Utamaduni na Sanaa ya Benin, Xi'an ni mji ambao wenye mambo mengi ya kale na wenye hali nyingi motomoto, wakati huohuo Benin yenyewe inajivunia rasilimali nyingi za kitamaduni na utalii zinazochanganya kina cha kihistoria na ustawi wa kisasa.
Kwa upande wake Zhang Wei, Balozi wa China nchini Benin amesisitiza kuongezeka kwa mawasiliano ya kitamaduni kati ya Xi'an na Benin katika miaka ya hivi karibuni, ikionyesha kuongezeka kwa kina kwa ushirikiano wa pande mbili.
Ameelezea matumaini kuwa China na Benin zitaendelea kufanya kazi pamoja ili kuimarisha ushirikiano wao wa kimkakati na kujenga mustakabali wenye matumaini.
Miujiza ya Wanyamapori: Kutoka Mbuga Tambarare za Afrika hadi Uwanda wa Juu wa Qinghai -Tibet, China
Mandhari ya Kipekee ya Karst katika Mkoa wa Guizhou yavutia watalii
Tamasha la kimataifa la densi lafunguliwa katika Mkoa wa Xinjiang, China likiwa na maonyesho 52
Wakulima wa China wawa na pilikapilika za uzalishaji wa kilimo katika kipindi cha Dashu
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma