

Lugha Nyingine
何时发放扶贫资金? 湖南官方年底前发放到位
Wataalamu wa Orbis na wanagenzi wa Rwanda wakifanya upasuaji ndani ya ndege ya Hospitali ya Macho ya Orbis (Orbis Flying Eye Hospital) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kigali mjini Kigali, Rwanda, Julai 29, 2025. (Picha na Cyril Ndegeya/Xinhua)
KIGALI - Rwanda imezindua programu ya matibabu na mafunzo ya wiki mbili ndani ya ndege ya Hospitali ya Macho ya Orbis (Orbis Flying Eye Hospital), hospitali ya kufundishia masomo kuhusu macho iliyopewa idhini kikamilifu kwenye ndege iliyobadilishwa matumizi ya MD-10, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kigali, mji mkuu wa Rwanda.
Hii ni mara ya kwanza kwa ndege hiyo ya hospitali ya Macho kutua nchini Rwanda ambapo jitihada hiyo inalenga kuimarisha ujuzi wa timu za wenyeji za huduma ya macho, kuongeza ufahamu kuhusu afya ya macho, na kupanua ufikiaji wa huduma za kuokoa uoni kote nchini humo.
Ndege hiyo ina chumba cha kisasa cha upasuaji, darasa na kituo cha hali ya juu cha kuigilizia uhalisia, ikiruhusu vyote matibabu ya kivitendo na elimu changamani ya matibabu. Orbis International, shirika lisilo la faida, linaendesha hospitali hiyo ya ndege duniani kote, likitoa huduma ya macho na mafunzo ya ubobezi kitaalamu kwa jamii ambazo zinakosa huduma husika.
Siku ya Jumanne, Waziri wa Afya wa Rwanda Sabin Nsanzimana alisisitiza haja ya nchi hiyo kuwa na wataalamu zaidi wa huduma ya macho.
“Rwanda kwa sasa ina madaktari wa macho 30 pekee kwa idadi ya watu zaidi ya milioni 13. Lengo letu ni kuongeza idadi hiyo kufikia angalau 70,” amesema.
Kama sehemu ya programu hiyo, wafanyakazi wa kliniki na wataalamu wa matibabu wa kujitolea wa Orbis wataongoza mafunzo yanayozingatia katika uigilizaji uhalisia, mazoezi ya vitendo ya upasuaji, na warsha maalum ambazo zitajikita katika ubobezi wa taaluma mbalimbali za macho, ikiwa ni pamoja na jicho butu (strabismus), upasuaji wa mtoto wa jicho, oculoplastics, na huduma ya matibabu ya retina.
Ciku Mathenge, mshauri wa matibabu wa Orbis barani Afrika, amezungumzia kuanzishwa kwa teknolojia ya kisasa ya uigilizaji uhalisia na ushiriki wa wataalam wa kimataifa, ambao utawezesha madaktari wa macho wa Rwanda kutoa huduma ya macho ya hali ya juu ndani ya jamii zao.
Amesema kuwa katika kipindi cha miaka minne iliyopita, shirika hilo la Orbis limetoa mafunzo kwa madaktari kutoka nchi mbalimbali za kanda hiyo, zikiwemo Kenya, Tanzania, Malawi, Ethiopia, Uganda, Nigeria, Zambia, na Burundi, katika mbinu kama vile matibabu ya leza na sindano za kingamwili za monokloni.
Upasuaji zaidi ya 40 unatarajiwa kufanywa kati ya Jumanne na Ijumaa ndani ya ndege hiyo ya hospitali na katika Hospitali ya Kibagabaga, kituo mwenyeji cha afya mjini Kigali. Tangu kuwasili kwao Julai 18, wataalamu wa Orbis tayari wametoa mafunzo kwa wafanyakazi zaidi ya 1,000 wa afya wa Rwanda, kwa mujibu wa waandaaji wa shughuli hiyo.
Picha iliyopigwa Julai 29, 2025 ikionyesha ndege ya Hospitali ya Macho ya Orbis (Orbis Flying Eye Hospital) iliyobadilishwa matumizi ya aina ya MD-10 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kigali mjini Kigali, Rwanda. (Picha na Cyril Ndegeya/Xinhua)
Waziri wa Afya wa Rwanda, Sabin Nsanzimana akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa programu ya matibabu na mafunzo ndani ya ndege ya Hospitali ya Macho ya Orbis (Orbis Flying Eye Hospital) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kigali mjini Kigali, Rwanda. (Picha na Cyril Ndegeya/Xinhua)
Mandhari ya Kipekee ya Karst katika Mkoa wa Guizhou yavutia watalii
Tamasha la kimataifa la densi lafunguliwa katika Mkoa wa Xinjiang, China likiwa na maonyesho 52
Wakulima wa China wawa na pilikapilika za uzalishaji wa kilimo katika kipindi cha Dashu
Maliasili nyingi za chumvi zaongeza mapato ya wanakijiji katika Wilaya ya Gegye, Xizang, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma